Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Brazil yamnyemelea Guardiola

Gadiola Pic Pep Guardiola

Tue, 13 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Shirikisho la soka Brazil (CBF) litawasiliana na Pep Guardiola kwa ajili ya kumshawishi Mhispania huyo achukue mikoba ya Adenor Leonardo Bacchi 'Tite' aliyejiuzulu.

Brazil inasaka kocha mpya atakayeziba pengo la Tite aliyejiuzulu baada ya Brazil kuondolewa kwenye robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Croatia.

Brazil iliondoshwa baada ya Rodrygo na Marquinhos kukosa penalti Croatia wakiibuka vinara na kutinga nusu fainali ambayo watacheza dhidi ya Argentina kesho.

Kwa mujibu wa ripoti iliyoandikwa na jarida ka SPORT, Brazil inataka kumng'oa Guardiola licha ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kukisuka kikosi cha Man City hadi mwaka 2025.

Rais wa shirikisho la Brazil, Ednaldo Rodrigues anayedili na masuala ya kuteua makocha, ataelewa kama Guardiola atagoma kuchukua mikoba ya Tite mwishoni mwa msimu wa 2022-20223 kwani mkataba wa Man City umembana kwa sasa.

Aidha Guardiola ndio chaguo namba moja anayependekezwa kuziba nafasi ya Tite kwani shirikisho la Brazil inatambua kocha huyo ana kiwango bora cha dunia kwasasa.

Chanzo: Mwanaspoti