Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Brazil yalazimishwa sare kufuzu Kombe la Dunia Qatar 2022

Brazil Vs Ecuador Mchezo huo ulimalizika kwa sare

Fri, 28 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya taifa ya Ecuador imetoa sare ya goli 1-1 na Brazil katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia Qatar 2022, mtanange uliopigwa Jana Alhamis.

Kwenye mechi hiyo, timu zote mbili zimemaliza mchezo wa dakika 90 zikiwa pungufu kufuatia wachezaji wake kuonyeshwa kadi nyekundu, ambapo mlinda mlango Alexander Dominguez alionyeshwa kadi kwa mchezo mbaya kabla ya Emerson Royal kuonyeshwa kadi pia dakika tano baadaye.

Brazil walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa kiungo mkabaji wa Real Madrid Casemiro kabla ya goli hilo kusawazishwa na Felix Torres kwa kichwa.

Brazil tayari wameshafuzu kucheza fainali hizo pamoja na Argentina wakati Ecuador wanashika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa kufuzu Kombe la Dunia Qatar kwa upande wa America Kusini Conmebol, ambapo timu nne za juu hufuzu moja kwa moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live