Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Brazil yaipiga Korea Kusini kama ngoma

Brazil Korea Wachezaji wa Brazil wakicheza Samba baada ya kuifunga Korea Kusini

Tue, 6 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya Brazil imeifunga Korea Kusini kwa bao 4-1 na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya kombe la Dunia nchini Qatar.

Beki mkongwe na nahodha wa Brazil, Thiago Silva ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kutoa pasi iliyozaa goli (Miaka 38, siku 74).

Mabao ya Brazil yamefungwa na Vinicius Junior dakika ya 7, Neymar Jr kwa mkwaju wa penati dakika ya 13, Richarlison dakika ya 29 na Lucas Paqueta dakika ya 36 huku bao la kufutia machozi la Korea Kusini likifungwa na Seung-Ho Paik dakika ya 76.

Tangu dakika za mwanzo, Brazil walionekana kuutawala mpira huku wakipiga pasi fupi na ndefu, kukimbia kwa kasi hasa wakati ambapo walishambulia jambo ambalo liliwqvuruga wapinzani wao na kusababisha kufanya makosa yaliyowagharimu na kupigwa 4G.

Mabingwa hao wa kihistoria katika michuano hiyo (wenye ubingwa wa Kombe la Dunia mara 5 - Brazil) watakutana na #Croatia katika Robo Fainali mnamo Desemba 9, 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live