Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Brazil wamheshimisha gwiji Pele

Peleeeeeee Brazil wamheshimisha gwiji Pele

Tue, 6 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya Brazil imeendeleza utamatuni wa kuheshimu mchango wa Magwiji wa Soka walioupiga mwingi katika kusaidia mafanikio ya Timu yao hapo zamani.

Hapa moja kwa moja huwezi sahau kumtaja Gwiji mahiri wa soka Edson Arantes do Nascimento alimaarufu kama Pele’.

Ni mchezaji aliyekuwa na mchango mkubwa sana katika muendelezo wa mafanikio ya Soka la Timu ya Taifa ya Brazil kwa kuifanya kutwaa Mataji Makubwa ikiwemo ya Kombe la Dunia.

Ikiunganisha na tukio la Nyota huyo aliyewahi tumikia kikosi cha timu hio ya Taifa ya Brazil ambaye kwa sasa hali yake ya kiafya haiko sawa kwa mujibu wa vipimo vya matibabu, akionekana kusumbuliwa na zaidi na Kansa, Timu ya Taifa ya Brazil ilichukua Dakika kadhaa za kuomba ili Gwiji huyo wa soka aweze rejea tena kuwa na afya njema.

Tukio la kushika picha kubwa na kuwa na utulivu wa muda kwa klabu hiyo lilifanyika baada ya kumalizika kwa dakika 90′ za mchezo wao dhidi ya Timu ya Taifa ya Korea ambapo waliibuka na ushindi wa jumla ya Goli 4-1 iliyofanya klabu hio kutinga vema hatua ya michuano ya Robo Fainali ya Kombe la Dunia inatakayoendele huko Qatar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live