Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Brazil waanza kuliamsha, wamtandika mtu 2-0

Brazil Waanza Kuliamsha, Wamtandika Mtu 2 0.jpeg Brazil waanza kuliamsha, wamtandika mtu 2-0

Fri, 25 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msimu huu kazi ipo! Mabingwa mara tano wa Michuano ya Kombe la Dunia, timu ya taifa ya Brazil imeanza rasmi Michuano hiyo ya mwaka 2022 inayoendelea nchini Qatar baada ya ushindi mabao 2-0 dhidi ya timu ya taifa ya Serbia.

Katika mchezo huo wa Kundi G, mabao ya ‘A Seleção’ yote yamefungwa na Mshambuliaji, Richarlison de Andrade kwenye dakika ya 62’ na 73’, Mshambuliaji huyo anacheza katika Klabu ya Tottenham Hotspur ya Uingereza.

Wababe hao wa Soka la Dunia wakiongozwa na Kocha wao Tite wakiwa na Nyota wao maarufu duniani, kina Neymar, Vinicius Jr, Raphinha, Casemiro, Alex Sandro, Marquinhos Thiago Silva, Golikipa Alisson aliwanyanyasa vilivyo Serbia hususani kipindi cha pili.

Mabingwa hao wa Michuano hiyo, mwaka 1958, 1962, 1970, 1994 na 2002 kwa sasa wanaongoza Kundi G wakiwa na alama zao tatu sawa na Switzerland katika nafasi ya pili, huku Cameroon wakiwa nafasi ya tatu na Serbia wakiburuza mkia bila alama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live