Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Brazil pigo tena! Jesus, Telles ndio basi tena Kombe la Dunia

Telles Jesus.jpeg Jesus, Telles ndio basi tena Kombe la Dunia

Sat, 3 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wawili wa Brazil Gabriel Jesus na Alex Telles wanatazamiwa kukosa michezo yote ya michuano ya kombe la Dunia iliyobaki katika kikosi cha Brazil baada ya kupata majeraha kwenye mchezo wa usiku wa jana dhidi ya Cameroon.

Jesus alipata maumivu ya goti huku Alex Telles akipata maumivu katika mguu wa kushoto.

Jesus na Telles wanaungana na Neymar Junior aliyeumia kifundo cha mguu kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Serbia, lakini Neymar anatazamiwa kurudi uwanjani kabla ya kombe la Dunia kumalizika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live