Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Brazil Yatwaa Medali ya Dhahabu michuano ya Olimpiki

Winger Wa Brazil,Malcom Akishangilia Goli La Ushindi Winger wa Brazil, Malcom akishangili baada ya kufunga goli la ushindi

Sun, 8 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya Brazil inayoshiriki michuano ya Olimpiki Mjini Tokyo,nchini Japan imeibuka mbabe kwa kushinda medali ya dhahabu baada ya kuivuruga Timu ya Taifa ya Hispania katika mchezo wa fainali uliopigwa siku ya jumamosi.

Mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Yokoham ulishuhudia Brazil ikitangulia kwa goli la Matheus Cunha kabla ya Oyzarbal kusawazisha na kusababisha mchezo huo kwenda muda wa ziada baada ya dakika 90 kuisha kwa sare ya goli 1-1.

Alikua ni Winger Malcom aliewahakikishia Brazil Medali ya dhahabu katika michuano hiyo baada ya kufunga goli la pili na la Ushindi katika dakika za nyongeza na kuifanya nchi hiyo kutetea medali yake kwa mara ya pili.

Wakati huo huo nahodha wa timu ya Brazil mkongwe Dani Alves,amezidi kuandika historia baada ya kuwa mchezaji aliebeba vikombe vingi zaidi katika ulimwengu wa soka likiwa ni taji lake la 44.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live