Sat, 30 Oct 2021
Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz
Mchezaji Paul Godfrey ‘Boxer’ wa Yanga amepewa pole kwa mara nyingine na wachezaji wenzake wakati wakiwa wanapasha miili joto kabla ya mchezo kuanza.
Wachezaji wa Yanga wakati wanaingia kupasha miili joto wote walikuwa wamevaa jezi yenye namba 14 ambayo anavaa Boxer.
Wote kwa pamoja walisimama kwa kupanga mstati na kuhesabu sekunde kadhaa kisha walijigawa na kuanza kurusha jezi kwa mashabiki.
Boxer wiki mbili zilizopita alifiwa na baba yake mzazi wakati yeye akiwa yupo kwenye majukumu ya klabu yake.
Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz