Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi wa Inter Milan anasema Onana atarudi

Andre Onana Ten.jpeg Bosi wa Inter Milan anasema Onana atarudi

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kipa wa Manchester United, Andre Onana anaweza kurejea Inter Milan siku moja kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo, Giuseppe Marotta.

Nyota huyo wa kimataifa wa Cameroon aliondoka Inter Milan na kujiunga na Manchester United kwa Pauni 47 milioni kipindi cha usajili wa kiangazi lakini ameanza vibaya akiwa na mashetani wekundu.

Kipa huyo amekosolewa na mashabiki kutokana na mfululizo wa makosa katika mechi, lakini bosi wa Inter akasisitiza anaamini siku moja atarejea Milan.

Hata hivyo, kocha Erik ten Hag amebaki kusimama na kipa wake aliyewahi kufanya kazi naye wakati anainoa Ajax.

Akiongea kwenye Tamasha la Michezo la Gazzetta dello, bosi wa Inter Milan Marotta alisema; “Lolote linaweza kutokea kwenye soka, hata kama wanaorejea hawana matokeo chanya kila mara. Ni kipa mzoefu na muhimu. Dili la Onana lilikuwa la mafanikio kwani tumepata faida baada kumpata bure.”

Inter ilimsajili kipa wa zamani wa Bayern Munich, Yann Sommer kama mbadala wa Onana baada ya kujiunga na Man United kiangazi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 amefurahia mwanzo mzuri wa maisha ya Serie A, akijizolea sifa nyingi kutoka kwa wachambuzi wa Italia.

Wakati huo huo, Onana alikosolewa na mkongwe wa Man nited Roy Keane kutokana na makosa anayofanya katika mechi: “Amekuwa na mwanzo mbaya sana. Kuwa kipa wa Man United ni kazi ngumu, unahitaji mtu mkubwa baada ya kufanya makosa. Tayari amefanya makosa machache, haukuwa mwanzo mzuri. Tumewaona makipa wengine ambao wamekuja wakiwa na sifa kubwa lakini wana makosa machache.”

Chanzo: Mwanaspoti