Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi wa Chelsea kufanya kufuru

Todd Boehly Jkl Mmiliki wa Chelsea, Todd Boehly

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mmiliki wa Chelsea, Todd Boehly amepanga kufanya maboresho uwanja wa mazoezi wachezaji wake wafurahie mazingira mazuri baada ya mazoezi ya kutwa nzima.

Mmiliki huyo alikutana na kocha anayeinoa timu hiyo Graham Potter kwaajili ya mipango hiyo na akaweka wazi anataka kujenga uwanja wa mazoezi wa kisasa wenye kila kitu ndani yake.

Mbali na uwanja kutakuwa na eneo la gym, bwawa la kuogelea maji, sehemu ya kuchezea pool na sehemu ya kufanyiwa matibabu wachezaji.

Tayari wataalamu wameshaajiriwa kwaajili ya kazi ya kuboresha ukuta mzima wa uwanja huo, lakini Potter anataka eneo lote liwe na mueonekano wa kisasa ambao utawajenga wachezaji kiakili kwa ujumla.

Kwasasa Chelsea ipo nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England huku Potter akiamini wachezaji wake watakua na furaha zaidi watakapotinga mazoezini kutokana na mazingira mapya.

Vile vile eneo zima la uwanja huo utapakwa rangi nyororo na kutakuwa na michezo mbalimbali kama 'Play Station' ili wachezaji wapate muda wa kupumzika baada ya mazoezi.

Mchakato wa ujenzi huo ulianza kwa siri kipindi cha fainali za Kombe la Dunia Qatar, vile vile kuna mpango mwingine wa kuboresha uwanja wa mazoezi wa timu ya wanawake wa Chelsea.

Chelsea imeshinda mchezo mmoja tu katika mechi 11 tangu fainali za Kombe la Dunia yalipomalizika huko Qatar, kwa mujibu wa ripoti mkurugenzi wa ufundi Christopher Vivell alionana na Potter katika uwanja wa mazoezi wa Cobham wanaofanyia wachezaji.

Potter alishutumiwa kuibadili Chelsea kuwa Brighton - kutokana na sasa rekodi zake na takwimu za uwanjani kufanana kabla ya kutoka kwenye timu hiyo na kutua Stamford Bridge.

Potter alitua kwenye kikosi cha The Blues kuchukua mikoba ya Thomas Tuchel, Septemba mwaka jana.

Maisha ya kocha huyo ni magumu licha ya kufanya usajili wa nguvu uliyogharimu kitita cha Pauni 600 milioni.

Takwimu zilionyesha Chelsea imeweka rekodi mbovu kama ilivyokuwa Brighton msimu uliyopita chini ya Potter kabla ya kujiunga na klabu hiyo inayomilikiwa na Boehly.

Kwasasa Chelsea inashika nafas 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa na pointi 31, wakifungwa mabao 23 na kuruhusu mabao 23 msimu huu.

Chanzo: Mwanaspoti