Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi wa Bayern atoboa siri nzito usajili wa Harry Kane

Harry Kane Germany Bosi wa Bayern atoboa siri nzito usajili wa Harry Kane

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bayern Munich Herbert Hainer amesema Harry Kane hakununuliwa kwa Pauni 104 milioni kama watu walivyodhania.

Iliaminika kwamba mabingwa hao wa kihistoria walimsajili walimsajili fowadi huyo kwa Pauni 104 katika dirisha la usajili la kiangazi.

Hata hivyo, Hainer amethibitisha kwamba usajili huo haukugharimu pesa nyingi baada ya kuweka wazi kiwango halisi alichonunuliwa.

Akizungumza kupitia FAZ bosi huyo alisema Kane alinunuliwa kwa Pauni 85 milioni baada ya kutimkia London kwa ajili ya Munich.

"Kane hakununuliwa zaidi ya Pauni 100 milioni- pesa itaongezeka endapo tutabeba ubingwa zaidi ya makombe matatu ndani ya misimu kadhaa. Imejumuisha na bonasi pia."

Kane amefiti katika maisha ya Ujerumani tangu alipotua na wikiendi iliyopita alihudhuria sherehe za Oktobafest kwa mara ya kwanza. Kane alivaa mavazi ya kitamaduni ya 'lederhosen' katika sherehe hiyo iliyosheheni mastaa wa Beyern.

Tangu alipotua Agosti, Kane alifunga mabao nane katika mechi saba alizocheza mashindano yote. Hata hivyo Ujerumani ilitengua hat-trick aliyofunga dhidi ya Bochum.

Kane alifunga mabao matatu katika ushindi wa mabao 7-0 lakini mabao hayo hayakufuatana ndio maana hat-trick hiyo ikatenguliwa kwa mujibu wa sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live