Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi Singida FG afunguka ishu ya Kakolanya, Kagoma

Beno Kakolanya Ew Beno Kakolanya

Wed, 29 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Zikiwa zimepita siku 44 tangu kipa wa Singida Fountain Gate, Beno Kakolanya adaiwe kutoroka kambini huku kukiwa na ukimya juu ya hatima yake, rais wa klabu hiyo, Japhet Makau amefunguka kinachoendelea kwa mchezaji huyo na kiungo, Yusuph Kagoma.

Yusuf Kagoma

Kakolanya alidaiwa kuondoka Kambini Aprili 14, mwaka huu saa chache kabla ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, ambapo Singida ilipoteza kwa mabao 3-0.

Klabu hiyo ilimtuhumu Kakolanya kutoroka Kambini kutokana na kujichukulia uamuzi wa kuondoka bila ruhusa maalum licha ya kukataliwa na viongozi wa timu hiyo wakimtaka asubiri mchezo huo umalizike, lakini akagoma.

Uongozi wa timu hiyo ulidai pamoja na hatua nyingine za kinidhamu utafanya uchunguzi kwenye suala la upangaji matokeo kwani amekuwa na tabia hiyo mara kwa mara.

Hata hivyo, akizungumza leo jijini Mwanza baada ya mchezo kati ya Singida FG na Kagera Sugar, Makau amesema nyota huyo ameshaitwa mara mbili kwenye shauri kusikilizwa, lakini hakutokea, huku akieleza kwamba watakwenda mbali zaidi kwa kufuata kanuni za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

"Suala la Kakolanya kuna taratibu zinaendelea tumemuita kwenye shauri tumeshamwita mara mbili hajafika na taratibu zake tunatakiwa tumwite mara tatu kama hajafika tunaripoti TFF kwamba hakuhudhuria kwenye shauri kwahiyo hatua zaidi zinachukuliwa katika hilo," amesema Rais huyo.

"Kuhusu Yusuph Kagoma hana shida yeye kuna taratibu tumemalizana naye hana tatizo lolote na mtamsikia anaibukia wapi katika msimu unaokuja."

Hata hivyo, akinukuliwa na Mwanaspoti Mei, mwaka huu, Kakolanya alisema baada ya kutojibu barua ya kuitwa kwenye kamati ya nidhamu aliondolewa kwenye kundi la WhatsApp la wachezaji wa timu hiyo huku nyumba yake akipewa mchezaji mwingine.

Aliongeza kwamba hajapewa barua ya kuonyeshwa kama amefukuzwa ama amesimamishwa kazi, hivyo viongozi wa klabu hiyo ndiyo wanaojua hatma yake

Akizungumzia hatima ya Kocha Ngawina Ngawina ambaye alikabidhiwa timu Machi 7, mwaka huu, Makau amesema, "tulimpa mkataba wa mpaka mwisho wa msimu tunaomba ripoti yake atuletee alafu tunaangalia tunajiandaaje kwa ajili ya msimu unaokuja."

Rais huyo amethibitisha kwamba baada ya msimu kumalizika klabu hiyo itafanya mchakato wa kubadilisha jina na kuondoa neno Singida na kuitwa Fountain Gate FC.

"Rasmi tutawataarifu lakini Singida muanze kuliondoa taratibu. Tutawataarifu rasmi lakini hii timu inakwenda kuitwa Fountain Gate FC na makazi yake yatakuwa Mwanza," amesema Makau.

Chanzo: Mwanaspoti