Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi Simba jeuri tupu Super Cup

KISPIKA CHA AHMED ALLY 1140x640 Ahmed Ally

Sat, 1 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amefunguka kuwa, michuano ya CAF Super Cup ambayo wanatarajia kushiriki msimu huu, ni hatua kubwa sana kutokana na upinzani wa klabu kubwa Afrika ambazo zitashiriki michuano hiyo.

Ikumbukwe kuwa, michuano hiyo ilizinduliwa Agosti 10, 2022 jijini Arusha katika mkutano mkuu wa kawaida wa 44 wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), huku Simba ikiwa timu ya kwanza kutoka Tanzania kuwa miongoni mwa zitakazoshiriki kuanzia Agosti mwaka huu.

Timu zingine ambazo zitashiriki michuano hiyo ni Al Ahly na Zamalek kutoka Misri, Raja Casablanca na Wydad Casablanca (Morocco), CR Belouizdad na JS Kabylie (Algeria) na Esperance (Tunisia).

Akizungumza nasi, Ally alifunguka kwamba: “Timu zote ambazo tutashiriki nazo kwenye michuano hii zimepata mafanikio makubwa sana ikiwemo kutwaa ubingwa wa Afrika.

“Kwa upande wetu hii ni hatua kubwa sana, kwa sababu ni mara yetu ya kwanza kushiriki lakini pia kwa rekodi zetu kwenye michuano ya kimataifa ni nzuri. Tumecheza robo fainali tatu kimataifa, kwa maana hiyo hii inadhihirisha kuwa tumeingia kwenye michuano ya wakubwa.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: