Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi Simba atamba "Robo fainali ni lazima"

Robertinho Vipers Simba Ahmed Ally

Tue, 28 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amefunguka kuwa, ushindi walioupata dhidi ya Vipers umewapa matumaini makubwa ya kufika hatua ya robo fainali kunako michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Jumamosi iliyopita, Simba ikiwa Uganda, iliibuka na ushindi wa bao 0-1 dhidi ya Vipers, ukiwa ni mchezo wa Kundi C la michuano hiyo.

Baada ya ushindi huo, Simba imefikisha pointi tatu ikicheza mechi tatu, inashika nafasi ya tatu nyuma ya vinara Raja Casablanca wenye tisa, Horoya (4) na Vipers wakiburuza mkia na pointi moja.

Ally alifunguka kwamba: “Ushindi wetu wa Uganda ni ishara kuwa kazi ya kuitafuta robo fainali inaanza, haitakuwa rahisi maana Vipers hawawezi kukubali kufungwa nje, ndani na Horoya hatokubali kupoteza matumaini yake.

“Lakini yote yanawezekana kama kila Mwanasimba atatimiza majukumu yake. Ajenda kuu ya kitaifa ya Wanasimba hivi sasa ni ‘Operations six points eye to the quarter finals’ (Mpango ni alama sita, jicho kwenye robo fainali).

“Kila mwenye silaha, mwenye mawazo na mwenye mbinu atumie ili kuhakikisha kuwa azma yetu ya kufika robo fainali kwenye michuano hii inatimia.”

KUNDI C

P W D L GF GA GD Pts

Raja CA 3 3 0 0 10 0 +10 9 Horoya 3 1 1 1 1 2 −1 4 Simba 3 1 0 2 1 4 −3 3 Vipers 3 0 1 2 0 6 −6 1

Chanzo: www.tanzaniaweb.live