Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi Simba amaliza utata Pacome na Chama nani bora

Pacome Chama Pc Bosi Simba amaliza utata Pacome na Chama nani bora

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage amesema kuwa kiungo mshambuliaji wa watani zao, Klabu ya Yanga, Pacome Zouzoua ni mchezaji mzuri lakini watu wasimfananishe na Clatous Chama kwani kila mmoja wao ni mzuri kutokana na aina yake ya uchezaji.

Rage amesema hayo kufuatia baadhi ya mashabiki kumfananisha Pacome na Chama huku wengine wakienda mbali zaidi na kusema kuwa Chama hamfukii Pacome hata nusu.

Juzi, Februari 24, 2024 Pacome alionyesha kiwango bora wakati yanga wakiifunga CR Belouizdad bao 4-0 na kutinga hatua ya robo fainali ya CAFCL wakiwa na mchezo mmoja mkononi, na kuvunja rekodi yao ya miaka zaidi ya 52 iliyopita kufika hatua hiyo.

Katika mchezo huo, Pacome alitengeneza nafasi tano kati ya 10 ambazo Yanga walitengeneza ambapo kwenye nafasi hizo, nafasi moja ilikuwa bao ambalo alifunga kennedy Musonda.

“Ukisema ball control na ball possession ni Chama, ukisema ball dribbling na fast ni Pacome, kwa hiyo ni wachezaji wawili tofauti.

“Pacome anakimbia sana na anaweza kukimbia na mpira kwa umbali mrefu. Chama sio mkimbiaji, ni slow but sure. Ni kama unavyotaka kumfananisha Maradona na Owen wakati wao,” amesema Mzee Rage.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live