Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi Simba: Tulieni, Yanga SC Wanakufa

Simbasctanzaniak Bosi Simba: Tulieni, Yanga SC Wanakufa

Wed, 8 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah Muhene ‘Try Again’, amesema kuwa Yanga ni watoto wadogo kwa Simba na timu yao ipo tayari kuchukua alama tatu, Desemba 11.

Try Again alisema wao wanauchukulia mchezo wao na Yanga kama michezo mingine wanayocheza kwenye ligi nakwamba suala la kupata ushindi kwenye mchezo huo ni zaidi ya asilimia 90.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Try Again alisema kila kitu kimeshakamilika kabla hata hawajasafiri kwenda Zambia na kilichobaki ni kwa upande wa wachezaji kutimiza majukumu yao ndani ya uwanja.

“Yanga kwetu ni timu ya kawaida, hatuna hofu nao hata kidogo, mchezo huo wa dabi tunaona kama mechi nyingine za ligi ambazo huwa tunacheza na timu kutoka nje na Dar es Salaam.

“Mipango imeshakamilika kilichobaki ni kwa wachezaji kutimiza majukumu yao ndani ya uwanja, tunajua kila kitu kuhusu wao na niwahakikishie Wanasimba, Yanga anakwenda kufa,” alisema Try Again.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live