Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi Man City afurahia klabu kugombea watu wao

Skysports Man City Khaldoon Al Mubarak 6192020 Bosi kubwa wa Manchester City, Khaldoon Al Mubarak

Wed, 12 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Bosi kubwa wa Manchester City, Khaldoon Al Mubarak amesema kwa namna klabu nyingine zinavyokwenda kuchukua watu wao inaonyesha dhahiri jinsi mabingwa hao wa Ligi Kuu England wanavyolikamatia soka la dunia kwa sasa.

Manchester United imeenda kuwachukua Omar Berrada kutoka Man City kuwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wapo na imemchukua pia aliyekuwa mkurugenzi wa akademia ya miamba hiyo ya Etihad, Jason Wilcox ambaye alipita pia Southampton - kwenda kuwa mkurugenzi wa ufundi.

Man United imemchukua pia Toby Craig, ambaye alikuwa mkurugenzi wa mahusiano kwenye klabu ya Man City kwa miaka minane, wao wanakwenda kumfanya kuwa ofisa mkuu wa kitengo cha mawasiliano.

Al Mubarak alisema kitendo cha uajiri cha Man City kipo vizuri baada ya kusaidia timu nyingine kupata watu wa maana.

“Kwa kusema ukweli, hili linanifanya kujivuna,” alisema Al Mubarak.

“Inaonyesha jinsi ulivyo bora kwenye kila idara. Napenda kutumia neno wahitimu, wachezaji wetu kwenye akademia, wachezaji wa kikosi cha kwanza, makocha, madaktari, kocha wa viungo na mabosi wakubwa, imeonyesha sisi ni timu bora duniani.”

Mubarak alisema maofisa wao wanaoondoka na kwenda kujiunga na timu nyingine: “Wanaondoka kwa heshima wakiheshimu kile ambacho klabu imewasaidia katika kufikia malengo makubwa ya kazi zao. Tumeendelea kubaki kuwa marafiki. Sisi tunaendelea kupambana kubakiza watu tunaotaka wabaki. Lakini, wakati mwingine huwezi kushinda kila vita, hivyo ndivyo maisha yalivyo.”

Chanzo: Mwanaspoti