Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi Kagera atangaza vita nyumbani

Meck Mexime.png Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime

Fri, 16 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema licha ya ratiba ngumu inayomkabili mbeleni ila atahakikisha anatumia vyema uwanja wa nyumbani.

Kikosi hicho kinajiandaa na michezo miwili migumu ya mzunguko wa pili katika Ligi Kuu Bara kikianza na ule wa kesho kitakapocheza na Azam ambayo imecheza michezo minane bila kupoteza kisha Desemba 21, kucheza na Simba Uwanja wa Kaitaba.

Akizungumza Maxime alisema michezo hiyo ni migumu kwao kutokana na ubora wa wapinzani wao japo malengo yao makubwa waliyojiwekea ni kuchanga vizuri karata ili kubaki na pointi zote tatu muhimu.

“Kwa sasa akili zetu zipo mchezo wa kesho na Azam, tulikuwa na mapumziko mazuri ambayo tuliyatumia kwa ajili ya kutengeneza fitnesi ya baadhi ya wachezaji ambao hawakupata muda mrefu wa kucheza,” alisema na kuongeza:

“Mchezaji wetu, Deogratius Mafie, ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu sasa ameanza mazoezi taratibu ya GYM na ni matumaini yetu siku sio nyingi ataungana na wachezaji wenzake kwenye kikosi,” alisema.

Mecky aliteuliwa kuifundisha Kagera Oktoba 30, mwaka huu na katika kipindi hicho amekiongoza kikosi hicho kwenye michezo sita ambapo kati ya hiyo ameshinda minne, sare moja na kupoteza mmoja kikiwa nafasi ya saba na pointi 21.

Chanzo: Mwanaspoti