Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi Kagera Sugar aitisha kikao kizito

Seif Nassoro Matthijs De Ligt.

Fri, 17 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kumaliza mchezo dhidi ya Simba Sc katika uwanja wa kaitaba, kikosi cha Kagera Sugar Football Club pamoja na Viongozi wa wote walipata wasaa wa kukutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda Cha Kagera Sugar Limited Mr. Nassoro Seif ambaye pia ndio Mmiliki wa Kagera Sugar Football Club.



Kikao kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kiwanda cha Kagera Sugar ambapo,mkurugenzi alizungumza mambo mengi ambayo kimsingi yalilenga sana katika uboreshaji pamoja na Mabadiliko makubwa ya kikosi kuelekea msimu ujao wa Ligi kuu ya NBCPL 2024/2025 ili waweze kuleta ushindani mkubwa katika ligi.

Pia, wachezaji pamoja na Viongozi walipata wasaa wa kuchangia machache katika kikao ambapo walizungumzia pia kuhusu maboresho makubwa ya kiutedaji kuelekea Msimu ujao maana dhamila yao kubwa ni kuchukua ubingwa na pia kushiriki mashindano ya kimataifa msimu ujao.



Aidha, wachezaji walimuahidi Mkurugenzi kufanya vizuri katika michezo iliyo salia ili kujiweka nafasi nzuri katika msimamo wa Ligi na kuepuka kucheza Playoff au kushuka daraja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live