Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi Chelsea kumrudisha Antonio Conte EPL

Conte Antonio Chelsea Antonio Conte

Fri, 7 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chelsea wanafikiria kufanya maamuzi ya kumchukua Antonio Conte kama tiba ya kudumu ya kikosi hicho licha ya kumchukua Frank Lampard kama kocha wa muda mpaka mwishoni mwa msimu huu.

Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Xavi Alonso ambaye yuko Bayer Leverkusen anatajwa kuwa anaweza kuchukuliwa Chelsea kurithi mikoba ya Graham Potter.

Leicester City inahitaji pauni milioni 50 kwa ajili ya kumuuza kiungo mshambuliaji wa England James Maddison, Tottenham Hotspur wako kwenye nafasi ya kushinda kinyang’anyiro hicho.

Inter Miami wako tayari kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kumshawishi Lionel Messi 35, kujiunga na timu hiyo akitokea Paris St-Germain.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live