Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi Brighton apagawa na usajili wa Chelsea, awaonya wafanya usafi

CEO Brighton And Hove CEO wa Brighton and Hove Albion, Paul Barber

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku mbili zilizopita, kuliibuka uvumi mkali kwenye mitandao ya kijamii kwa timu ya Chelsea kwa mara nyingine tena ilikuwa inapanga njama ya kuwapokonya Brighton & Hove kocha wao, Muitaliano Roberto De Zerbi.

Itakumbukwa kwamba miezi michache iliyopita, De Zerbi aliteuliwa kama kocha mpya wa Brighton baada ya Chelsea kuwapokonya Brighton kocha wao Muingereza Graham Potter ambaye rekodi yake katika klabu hiyo la London haijakuwa nzuri tangu kumalizika kwa mechi za kombe la dunia nchini Qatar. Baada ya uvumi wa uvamizi wa Chelsea katika kambi ya Brighton tena, Afisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo amezungumza na kuonekana kutupa madongo kwa Chelsea kwa njia ya kejeli.

Paul Barber alisema kwa kejeli kwamba huwa anapenda sana kuzipokea simu kutoka kwa uongozi wa timu ya Chelsea wakati wanazungumzia mambo tofauti lakini ikifika kwenye maswala ya simu ya kuomba huduma za kocha wao, hapo ndipo anachora mstari mkubwa wa kujitenga na simu za Chelsea.

“Nina furaha kuchukua simu kwa Chelsea mbali na wakati ni kwa ajili ya makocha wetu," Barber aliiambia FTLive, kulingana na mwanahabari wa habari za michezo, Fabrizio Romano.

Barber pia alizamisha mkuki wa kejeli kwenye nyoyo za mashabiki wa wapenzi wa Chelsea akisema kwamba hata ameshatoa tahadhari kwa wafanyakazi wa usafi katika timu hiyo kuwa macho kwani Chelsea wanaweza wasajili wakati wowote bila habari yake.

"Nimewaambia wafanyikazi wa usafi kuwa waangalifu, wanaweza kuwindwa pia," Paul Barber aliongeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live