Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi Barca anateseka Madrid kushangilia

Real Madriddddddd Bosi Barca anateseka Madrid kushangilia

Sun, 9 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mambo ni moto. Aliyekuwa rais wa Barcelona, Joan Gaspart ameponda vikali kitendo cha Real Madrid kushangilia ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kufanya sherehe siku mbili mfululizo.

Baada ya kushinda taji hilo baada ya kuichapa Borussia Dortmund 2-0 katika fainali iliyofanyika Wembley, Juni 1, wachezaji wa Real Madrid pamoja na mashabiki wao walifanya sherehe kwa siku mbili, Jumapili na Jumatatu katikati ya jiji la Madrid, huku wakishangaza pia na sherehe za kubeba taji la La Liga kwa msimu huu.

Gaspart alisema juu ya sherehe hizo: “Nilitazama sherehe zao zote. Nilitazama kupitia RMTV. Nilitazama kuona ni jinsi gani sisi tutashangilia mwakani. Sikufurahia, lakini nilitazama.

“Wanajua namna ya kushangilia wanapishinda ubingwa. Sisi tunapopoteza tunaumia sana, tunaposhinda, tushangilia kawaida sana. Wao wanashangilia utadhani wamefika mwezini au utadhani wameshinda kitu cha ajabu. Sisi tumekuwa tukishangilia kwa tahadhali, hebu tujiachie.

“Wajuu zangu waliniuliza ‘Mnashida gani nyie?’ Kazi kwetu sasa tuendelee kuomboleza au tusimame imara kwa ajili ya mapambano.”

Chanzo: Mwanaspoti