Tue, 20 Feb 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mkurugenzi wa zamani wa soka wa Azam FC, Mromania Mario Marinica ametangazwa kuwa Kocha Mkuu mpya wa timu ya Taifa ya Liberia kwa mkataba wa miaka miwili.
Mojawapo ya masharti ambayo amepewa ni kuiwezesha timu ya Taifa ya Liberia kufuzu katika Mashindano ya AFCON 2025 nchini Morocco.
Mara ya mwisho kwa kocha huyo mwenye umri wa miaka 59 aliiongoza Malawi ambapo aliiwezesha kutinga hatua ya 16 bora kwenye AFCON mwaka wa 2021.
Mario alihudumu kama Mkurugenzi wa soka (Director of Football) ndani ya Azam FC ya Tanzania 2015-2016.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live