Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi Azam FC aukubali mziki wa Simba, afunguka kilichowaponza

Simba Wakishangi.jpeg Simba wakishangilia.

Fri, 10 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Azam FC, Zakazakazi amesema wamekubali wamecheza chini ya kiwango na kugusia kwamba katika mchezo wa jana Simba SC wamekuwa na siku nzuri hivyo kuwa sababu ya kupoteza kwa kufungwa goli 3-0 dhidi ya Simba SC.

“Kukosa namba 9 asilia kwenye timu yetu hakujatugharimu chochote kwenye mchezo huu kwa sababu mechi takribani asimilia 80 za msimu huu tumecheza bila straika asilia na tumeshinda mabao mengi kuliko tulipokuwa na straika. Tumepoteza mchezo mmoja tofauti na michezo ambayo tumepoteza tukiwa na straika kwa hiyo, hiyo sio sababu.

“Tumepoteza kutokana na kushindwa kuamua mechi wakati ambao tulitakiwa tuamue mechi. Kipindi cha kwanza tulitakiwa tumalize nafasi lakini tukashindwa, Simba wametumia nafasi wametuadhibu. Niwapongeze Simba kwa matokeo haya.

“Huwezi kusema tuko kwenye vita ya nafasi ya pili, vita sio kubwa sana, vita ni kumaliza katika nafasi ya juu kadri inavyowezekana. Uwezekano wa kucheza kimataifa msimu ujao upo kwa sababu mechi bado zipo na chochote kinawezekana.

“Simba wametufunga walikuwa na siku nzuri sana leo (jana), lakini wanaweza kuwa na siku mbaya mechi moja wakapoteza na sisi tukapata nafasi ya kukaa juu,” amesema Zakazakazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live