Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Borussia Dortmund Kukamilisha Dili la Adeyemi

Adeyami Karim Adeyemi

Tue, 10 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Borussia Dortmund wanakaribia kukamilisha dili la mshambuliaji wa RB Salzburg, Karim Adeyemi ili kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Erling Haaland anaetarajiwa kuondoka majira ya kiangazi.

Taarifa zinasema Makaratasi na mikataba inaandaliwa wiki hii kati ya Borussia Dortmund, RB Salzburg na Karim Adeyemi kwaajili ya kukamilisha dili hilo.

Makubaliano ya mdomo yalifikiwa miezi kadhaa iliyopita kwani kipaumbele cha Adeyemi kilikuwa kujiunga na Borussia Dortmund licha ya ofa nyingi alizopata.

RB Salzburg itapokea ada ya takriban €38m pamoja na nyongeza, huku Adeyemi akitia saini mkataba wa muda mrefu na kifungu cha NO cha kutolewa kikiwamo.

Adeyemi amefunga mabao 23 katika mashindano yote msimu huu akiwa na RB Salzburg na anachukuliwa kuwa mmoja wa washambuliaji mahiri katika soka la Ulaya.

Adeyemi atakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa Borussia Dortmund kuelekea msimu ujao baada ya Niklas Süle na Nico Schlotterbeck kutangazwa mapema wiki iliyopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live