Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Boniface Mkwasa alisajiliwa Simba 1982

Mkwasa M Boniface Mkwasa alisajiliwa Simba 1982

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni mwaka ambao ulikuwa na matukio mengi yenye utata katika usajili katika Ligi ya Daraja la Kwanza Tanzania Bara (sasa Ligi Kuu).

Kiungo mahiri wa Yanga Africans (sasa Yanga SC), Charles Boniface (kabla hajaanza kulitumia rasmi jina la Mkwasa) alizua taharuki kubwa baada ya kubainika alikuwa amesajili Simba.

Hata hivyo, Charles Boniface hakuwa mchezaji pekee  aliyeingia kwenye matatizo ya usajili mwaka huo kulikuwa na wachezaji takribani wanane ambao usajili wao ulienguliwa na FAT (sasa TFF).

WENGINE WANANE NAO Mbali na Charles Boniface, wachezaji wengine nao waliingia kwenye utata wa kuzitumikia timu zao mpya.

Kiungo Hussein Ngulungu alikuwa amejaza fomu kuitumikia Pan Africans baada ya kuachana na Tumbaku ya Morogoro lakini usajili wake uligomewa.

Chama cha Soka cha Tanzania kilimpitisha Boniface kuitumikia Simba na Ngulungu alibakishwa Tumbaku.

Hata hivyo, Ngulungu alizaja fomu za kuachana na Tumbaku Septemba 27, 1981 na miezi mitatu baadaye (Desemba 3, 1981) aliacha kazi katika Mamlaka ya Tumbaku iliyokuwa ikiimiliki timu hiyo.

FITNA ZA MPIRA Inadaiwa Tumbaku ilifanya fitna za kimpira na kuchelewesha fomu zake za kuhama kwa makusudi ili aendelee kuonekana ni mchezaji wao halali.

Mchezaji mwingine aliyefanyiwa fitna kama hizo ni Abdallah Burhani aliyekuwa akitaka kuhamia Pan Africans kutoka Biashara ‘RTC’ Kagera.

FAT ilikataa kumhidhinisha kuitumikia Pan kwasababu fomu zake za uhamisho hazikuwa na saini ya klabu yake ya zamani, Biashara na Chama cha Mpira Wilaya ya Bukoba.

Inadaiwa mshambuliaji huyo mwenye nguvu, alikuwa anadaiwa na klabu yake ya Biashara, hivyo nayo ikachelewesha fomu zake ili asionekane kama amehamia Pan Africans.

Burhani alikiri kwamba alikuwa  na deni la bishara lakini alishaamua kuachana na timu hiyo.

BONIFACE AKIRI, AKATAA Tukirudi kwa Boniface alikiri kusaini Simba, lakini aliitaka FAT ambayo ilimuidhinisha kuitumikia timu hiyo, isizitambue fomu za timu hiyo. Mchezaji huyo aliandika barua kwa chama hicho na kuitaka imtambue yeye kama mchezaji wa Yanga. Hata hivyo, FAT iliigomea barua hiyo na kumtambua Boniface kama mchezaji mpya wa Simba aliyetokea Yanga.

Baada ya sintofahamu hiyo, Simba na Yanga zilikuwa zikijiandaa kulifikisha suala hilo katika Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

ELISHA JOHN APELEKWA SIMBA Mwaka huo pia Simba ilihusika katika usajili wa kiungo mwingine wa Coastal Union, Elisha John. FAT ilimhidhinisha kiungo huyo kuitumikia Simba, lakini Wagosi wa Kaya hawakukubali walidai bado alikuwa mchezaji wao.

Katika usajili wa mwaka huo, Simba nayo ilizuiwa kuwatumia wachezaji watatu Malota Soma, Thobias Nkoma na Ibrahim Marekano.

MALOTA, NKOMA KAMA NGULUNGU Malota na Nkoma walikuwa wanatoka kuitumikia Tumbaku ya Morogoro ya Morogoro na FAT iliwaidhinisha kuitumikia timu yao ya zamani badala ya Simba. Marekano alitakiwa kurudi kuitumikia timu yake ya Asante Kotoko ya Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Sakata la Malota na Nkoma lilikuwa kama lile la Ngulungu aliyetaka kuiacha Tumbaku na kusajili Pan Africans nao walihesabika kuchelewa usajili kwa kuwa fomu zao hazikuwa zimekamilika kutoka Tumbaku.

Hata hivyo, wachezaji hao waliamua kubaki Simba na kukubali kucheza michezo ya kirafiki tu. Malota na Nkoma walishaacha kazi katika Mamlaka ya Tumbaku na hawakujaza fomu za usajili za timu hiyo kwa ajili ya msimu huo.

MAREKANO ALITOA KALI Kitu cha kushangaza, kwa upande wa winga Ibrahim Marekano alidai hata makao makuu ya klabu ya Asante Kotoko alikuwa hayafahamu.

Ilidaiwa mara ya mwisho Marekano alicheza ligi mwaka 1979 akiwa na timu ya Usagishaji (NMC) ya Tabora. Baada ya hapo aliitumikia timu ya Benki ya Biashara ambayo haikuwa ikishiriki ligi yoyote. Naye aliamua kubaki Simba  na kucheza mechi za kirafiki tu.

SUNDAY JUMA NAYE AZUIWA Simba pia iliingia katika utata wa mchezaji mwingine, Sunday Juma ‘Pikipiki’ ambaye FAT ilimtaka abaki kuitumikia timui yake ya Kibo Shooting ya Moshi, Kilimanjaro ingawaje alimwaga wino kuitumuikia Simba. 

Winga huyo aliyekuwa na kasi uwanjani alikuwa amepata uhamisho wa kikazi kutoka RTC Moshi na kuja kufanya kazi RTC Dar es Salaam.

Nini kilimbakisha Boniface kuendelea kuitumikia Yanga? Usikose wiki ijayo. Nini kilimbakisha Boniface kuendelea kuitumikia Yanga? Usikose wiki ijayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: