Pape Osman Sakho, Raia wa Senegal msimu huu alisajiliwa na Club ya US Quevilly-Rouen Métropole nchini Ufaransa, akitokea Simba Sc, nenda kasome hizo Comments za Watanzania (Wanasimba) kwenye hiyo page ya Club unaweza fikiri Sakho ni Mbongo, Hadi Baadhi ya Comments za wachambuzi mahiri nilizikuta mule
Fiston Kalala Mayele, akasajiliwa Pyramid Fc ya nchini Misri, nenda kasome hizo Comments za Watanzania (Wanayanga) kwenye Page ya Pyramid nenda kaangalie Page ilivyofurika Watanzania.
Akasajiliwa Baraka Majogoro pale nchini South Africa na Klabu ya Chippa United inayoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo akitokea KMC, na waliyowengi walijua lakini no one care, wachambuzi wengi hawakupost kabisa wakiamini Baraka Majogoro siyo content.
Mohammed Ouattara akasajiliwa na moja ya klabu bora huko Uarabuni, lakini Kenedy Juma Bado yupo Simba Sc, Mwamnyeto Bakari, Dickson Job, nenda YouTube search Mohammed Ouattara utakutana na clip za page mbali mbali za nchini Ivory coast zikimpost na kumpamba, njoo huku kwetu search Dickson Job, ukutane na maandiko yakimponda mara mfupi mara mipira ya juu hawezi mambo mengi yakupondeana.
Lakini search Clatos Chota Chama, ukutane na maandiko yake, clip zake zilimuelezea vizuri, ishazoeleka yaani, media na wachambuzi tunao toa michango chanya kwa wachezaji wetu wazawa ni wachache sana sanaaaa, muda mwingine sisi wachambuzi na media tunachangia mnoo kurudisha nyuma hawa wachezaji wazawa.
Kuna mchezaji wa kagera Sugar alienda kwenye majaribio Ubelgiji wangapi tunajua kuhusu yeye, lakini leo hii tusikie kasajiliwa KRC Genk, siku anarudi Tanzania waandishi wa habari tunaweza kulala Airport kwaajili ya kupata tu interview na yeye
Kila siku kwenye media kubwa wao ni Chama , Aziz Ki , lakini Ukija kwenye Top scorer wa ligi kuu hadi sasa Feisal, eti hazungumziwi kisa alifunga wachezaji wakiwa pungufu kwa hiyo mlitaka apate nafasi akose? Hapo napo ndo ungekuwa mjadala mkubwa.
Tunajikuta tuna upendo wa juu sana na wachezaji wa kigeni na tunawapa full ushirikiano lakini likija suala la native player tunawaona hawana dili, Hata huyo Samatta mwenyewe, wengi hatumheshimu na hatumpi heshima anayostahili.