Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bongo hakuna kama Chama

Chama Yanga 003 Bongo hakuna kama Chama

Mon, 1 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa jinsi alivyoyateka maeneo yote ya nchi kupitia media mbalimbali (Online media's, radio's TV's nk)kwa zaidi ya mwezi mzima sasa imeonyesha umma wa Tanzania na Africa mashariki kuwa hakujawahi kutokea mchezaji Bora wa kigeni zaidi ya Clatous Chota Chama.

Ile kampeni ya kumlinganisha na kila kiungo anayekuja kucheza ligi ya hapa imekwisha. Hakuna cha Pacome, Fei, Niyonzima, Kipre, wala nani Chama amebaki kuwa juu Yao kitakwimu, kiuwezo, kimafanikio, nk.

Yes amefanya makubwa na amedhihirisha hilo kwa misimu mingi ndani ya ligi yetu tangu 2018 alipoletwa nchini na kusajiliwa na Simba chini ya usimamizi wa Zacharia Hanspop (marehemu).

Tayari mwamba wa Lusaka amesaini mkataba wa kuitumikia Yanga akitokea Simba ambako amedumua kwa misimu saba.

Utamchukia kwa lipi Chama? Club zote nchini zinatamani kuwa na Chama na wala sio mchezaji mwingine. Bahati mbaya hawezi kuzitumikia zote kwa wakati mmoja bali ikiwa upande wa Simba utatosheka na huduma yake basi ataenda kwa wengine na wao wa enjoy kumuona na jezi Yao.

Kila #Mwanasimba anayohaki kujivunia mazuri ya Chama na kumtakia kila lenye kheri ikiwa ataondoka kwa maana amefika katika kilele cha ubora akiwa Simba hivyo hakuna cha zaidi anachoweza kuisaidia Simba zaidi ya kuibakisha palepale penye kilele cha mafanikio.

Clatous Chota chama ndio mchezaji alietoa pasi nyingi za mabao [assists] tangu msimu wa 2020/21.

Ametoa jumla ya assists 35.

Hawa hapa Wachezaji wenye assists nyingi katika Nbc Premier League tangu mwanzoni mwa msimu wa 2020/21

35 — Clatous Chama

23 — Said Ntibazonkiza

22 — Shomari Kapombe

17 — Abdulrahman Mussa

15 — Mohamed Hussein

15 — Kibu Denis

14 — Kipré Zunon

14 — Luis Miquissone

13 — Feisal salum

13 — Prince Dube

12 — Stephane Aziz Ki.

Mnapoambiwa kwenye hii Ligi Kuu Tanzania hajawahi kutokea mchezaji kama Chama Jr, elewa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live