Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bologna na hatma ya Uefa mbele ya jini mla watu

Lautaro Martinez Mahakama Lautaro Martinez

Sat, 9 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ligi Kuu Italia inatarajiwa kuendelea leo ambapo mmoja kati ya michezo inayotarajiwa kuvuta watu wengi ni ule kati ya Bologna na Inter Milan.

Mchezo huo unaonekana kuwa mmoja kati ya mechi ambazo zimeshika hatima ya Bologna kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao kwa kumaliza kwenye nafasi nne za juu.

Bologna itakutana na Inter Milan iliyo kwenye kiwango bora msimu huu ambapo ikiwa ndiyo kinara wa Serie A.

Matokeo ya ushindi yatakuwa na maana kubwa kwa Bologna kwa sababu ikifungwa itakuwa imeweka tofauti ya alama mbili kati yake na Roma inayoshika nafasi ya tano ikiwa itashinda mechi ya wikiendi hii, huku ikitoka sare.

Inter Milan ambayo inaongoza ikiwa na pointi 72 itahitaji kushinda ili kuweka pengo kubwa zaidi la alama kati yake na Juventus iliyo nafasi ya pili.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Renato Dall’Ara kuanzia saa 2:00 usiku.

Mbali ya mchezo huo wa leo, ligi hiyo pia itakuwa na michezo kadhaa ambapo Sassuolo itacheza dhidi ya Frosinone, wakati Cagliari ikicheza dhidi ya Salernitana zote hizi zitapigwa saa 11:00 jioni leo.

Mchezo wa mwisho kwa leo ni kati ya Genoa na Monza utapigwa saa 4:45 usiku.

Kesho kutakuwa na mechi nne lakini unaoonekana kuwa mkali ni ule wa Juventus dhidi ya Atalanta utakaopigwa saa 2:00 usiku.

Mechi hii kwa Atalanta itakuwa ndio tiketi ya kupanda hadi nafasi ya tano ambayo itawawezesha kufuzu michuano ya Europa ambapo itaishusha Roma iliyo kwenye nafasi hiyo ikiwa matokeo yao hayatokuwa mazuri.

Pia kwa Juventus ambayo inaikimbizia Inter kwenye mbio za ubingwa itahitaji kushindi ili kupunguza utofauti wa alama kati yao na hao Inter.

Mechi ya mapema itakuwa ni kati ya Lecce na Verona itaanza saa 8:30 mchana, AC Milan na Empol mechi itaanza saa 11:00 jioni wakati Fiorentina ikiumana na Roma saa 4:45 usiku, Jumatatu kutakuwa na mechi moja kati ya Lazio na Udinesse itakayopigwa muda kama huo. Tusubiri kuona maajabu.

Chanzo: Mwanaspoti