Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bolasie ajiunga timu ya 15

Yannick Bolasie Staa Yannick Bolasie

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Staa Yannick Bolasie amewapiga watu sapraizi baada ya kujiunga na klabu ya 15 katika maisha ya soka.

Klabu iliyopanda daraja hivi karibuni huko Brazil, Criciuma imenasa huduma ya winga huyo wa zamani wa Crystal Palace na Everton mwenye umri wa miaka 34.

Mashabiki kwenye mitandao ya kijamii wamempigia saluti mkali huyo wa zamani wa DR Congo kwa kile alichokifanya kwenye Ligi Kuu England na sasa anakwenda kufanya yake Brazil.

Shabiki mmoja alisema: "Huu jamaa amezuru dunia."

Winga huyo mzaliwa wa Ufaransa mwenye kimo cha futi 6 na inchi 2 ilikuwa hajawahi kucheza nje ya Ulaya. Na gwiji wa masuala ya usajili, Fabrizio Romano alisema Bolasie, alikwenda Criciuma kukamilisha masuala ya kufanyiwa vipimo vya afya juzi Jumatatu.

Klabu hiyo isiyofahamika sana duniani, ilipata mafanikio mwaka 1991 iliponyakua Kombe la Brazil.

Lakini, Criciuma ni timu kubwa kwenye Jimbo la Santa Catarina, ikiwahi kushinda ubingwa wa Serie B mwaka 2002 na Serie C miaka minne baadaye.

Sasa Bolasie ana matumaini ya kwenda kufanya kweli huko Criciuma, na uwanja wao wa Estadio Heriberto Hulse una uwezo wa kuchukua mashabiki 19,900.

Winga huyo aliachana na Swansea City, Januari mwaka huu. Hillingdon Borough ndiyo iliyokuwa timu ya kwanza ya Bolasie mwaka 2006, kisha alicheza Floriana, Plymouth Argyle, Rushden & Diamonds, Barnet, Bristol City, Palace, Everton, Aston Villa, Anderlecht, Sporting Lisbon, Middlesbrough na Caykur Rizespor.

Chanzo: Mwanaspoti