Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Boka awashusha presha Wananchi

Chadrack Boka Dfbs Chadrack Boka

Tue, 23 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Beki mpya wa Yanga, Chadrack Boka amewashusha presha mashabiki wa timu hiyo baada ya wikiendi iliyopita kupata maumivu katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Augsburg ya Ujerumani, huku akifichua alichoelezwa na mshambuliaji Mkongomani wa Wajerumani hao, Samuele Essende.

Boka aliyesajiliwa Yanga msimu huu akitokea FC Lupopo ya DR Congo, alipata majeraha hayo katika kipindi cha pili cha mchezo huo wa kirafiki yaliyomfanya aombe kutoka na timu yake kufungwa mabao 2-1 kwenye mechi iliyofanyika Uwanja wa Mbombela nchini Afrika Kusini.

Akizungumza na Mwanaspoti akiwa Afrika Kusini, Boka amesema alipata maumivu kutokana na kutopasha viungo kwa muda mrefu kabla ya mechi, huku hali ya hewa pia ikichangia kuumia kwake.

Alisema alipata mshtuko wa nyama za paja wakati anapambana kukaba na ilitokea kwa sababu hakupata joto sawasawa wakati anataka kuingia uwanjani.

“Sikuumia sana ni mshtuko tu ndio maana niliomba kutoka mapema ili nisizidi kuumia. Ila, kwa sasa niwatoe hofu niko salama na nimeshaanza kufanya mazoezi binafsi, hivyo mnaweza kuniona uwanjani mchezo ujao,” alisema Boka anayecheza beki wa kushoto.

ESSENDE Katika hatua nyingine, Boka alisema baada ya mechi  alizungumza na Mkongomani mwenzake anayechezea Augsburg, Samuele Essende ambaye aliitoa jasho safu ya ulinzi ya Yanga iliyoongozwa na Dickson Job pamoja na Ibrahim Bacca.

“Aliniambia mimi na Maxi (Nzengeli), kwamba Yanga ni timu kubwa na wachezaji wengi wa timu yao wameshangaa sana kuona wachezaji wenye uwezo mkubwa kama wao wakicheza Tanzania.

“(Essende) alisema tunacheza mpira wa kisasa na wa ushindani kama tutafanya vizuri Afrika na kucheza kama tulivyocheza nao, basi tutafika mbali zaidi kwani mpira unatazamwa sana duniani,” alisema Boka.

Essende anayechezea kikosi cha kwanza katika timu ya Taifa ya DR Congo akimuweka nje, Fiston Mayele ambaye msimu wa 2022/23 alichukua tuzo ya Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara kabla ya kutimka.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: