Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi yafuta mechi za usiku, Simba na Yanga

Bodisimba+picha Bodi yafuta mechi za usiku, Simba na Yanga

Fri, 23 Oct 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Oliver AlbertMechi za Simba na Yanga hasa zilizokuwa zifanyike kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 usiku, sasa zote zitafanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Bodi ya Ligi imetangaza hivyo.

 

Tayari Yanga walishaanza kutumikia uamuzi huo baada ya mechi yao ya jana dhidi ya Polisi Tanzania iliyokuwa imepangwa kufanyika saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Mkapa kuchezwa saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Uhuru.

 

Mechi nyingi za Simba na Yanga zilipangwa kuanza saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Mkapa lakini sasa zote itabidi zichezwe saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Uhuru kutokana na uwanja huo kutokuwa na taa za uwanjani  mbazo zinakidhi mechi kuchezwa usiku.

 

Chanzo: mwanaspoti.co.tz