Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya waamuzi yalaani unyanyasaji dhidi ya mwamuzi Taylor

Bodi Ya Waamuzi Yalaani Unyanyasaji Dhidi Ya Mwamuzi Taylor Bodi ya waamuzi yalaani unyanyasaji dhidi ya mwamuzi Taylor

Fri, 2 Jun 2023 Chanzo: Bbc

Bodi ya waamuzi PGMOL inasema inashangazwa na unyanyasaji "usio na msingi na wa kuchukiza" uliotekelezwa dhidi ya Anthony Taylor katika Uwanja wa Ndege wa Budapest kufuatia fainali ya Ligi ya Europa Jumatano.

Muingereza huyo ndiye aliyekuwa mwamuzi wa mchezo huo, ambapo Sevilla waliwafunga Roma kwa mikwaju ya penati baada ya timu hizo kutoka sare 1-1

Taylor na familia yake walizomewa na mashabiki wenye hasira kwenye uwanja wa ndege.

Maafisa wa uwanja wa ndege wa Budapest walisema raia wa Italia aliyehusika katika tukio hilo amefunguliwa mashitaka ya uasi.

Katika video hiyo ambayo imesambazwa kwenye mitandao ya kijamii, Taylor na familia yake wanashangiliwa na mashabiki huku wakisindikizwa kupitia uwanja wa ndege. Kisha ghasia k kuzuka wanapotoweka kupitia mlango ulio salama na wakatupiwa kiti.

Kufuatia mchezo huo, meneja wa Roma Jose Mourinho alionekana kwenye eneo la kuegesha magari akikabiliana na Taylor kwa maneno machafu.

Taarifa ya Uwanja wa Ndege wa Budapest ilisema: "Mashabiki wa timu ya Roma iliyoshindwa walimtambua mwamuzi katika eneo la chakula la uwanja wa ndege, ambapo alikuwa akisubiri ndege yake iondoke.

“Tunashukuru kwa ushirikiano wa karibu wa afisa mkuu wa uwanja wa ndege na polisi na kuongezeka kwa askari polisi uwanjani hapo wakati wa kuwasili na kuondoka kwa mashabiki, mamlaka iliingilia kati mara moja, na muamuzi alipelekwa kwenye chumba cha mapumziko na kupanda ndege yake salama, akiongozana na maafisa wa polisi.

"Raia wa Italia aliyehusika katika tukio hilo alikamatwa na polisi na kesi ya jinai imefunguliwa kwa tuhuma za uasi.", ilisema taarifa hiyo.

Msemaji wa Primia Ligi aliongeza kuwa: "Hakuna mtu anayepaswa kuteseka na tabia isiyo na sababu ambayo alilazimika kuvumilia.

Chanzo: Bbc