Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya ligi `yaibeba’ Namungo

24af53cddf361fc4bdff47240d8ec4f3 Bodi ya ligi `yaibeba’ Namungo

Sat, 13 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imesogeza mbele michezo miwili ya Namungo ikiwemo ule ujao dhidi ya Gwambina uliotakiwa uchezwe Machi 17, mwaka huu kuwapa nafasi ya kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids.

Akizungumza Dar es Salaam jana Mtendaji wa Bodi hiyo, Almas Kasongo aliyeongozana na timu hiyo kutoka Morocco alisema Namungo haina muda wa kucheza viporo inatakiwa kujiandaa na mchezo huo ujao wa kimataifa.

“Tulirekebisha mechi zote za Namungo utaona walikuwa wacheze tarehe 11, lakini tarehe 10 walicheza na Raja Casablanca na wamerejea tarehe 12 halafu tarehe 17 walikuwa na mchezo wa kimataifa na wa ligi zimegongana kwa hiyo tumesogeza mbele kuwapa nafasi,”alisema.

Alisema kutokana na jukumu hilo Namungo na Simba watakuwa na ratiba ngumu huko mbele kwa kucheza viporo na michuano hiyo ya kimataifa ili kwenda sawa na kumaliza ligi kwa wakati.

Namungo tayari wamerejea Dar es Salaam jana wakitoka Morocco katika mchezo wa kwanza wa makundi waliofungwa bao 1-0 dhidi ya Raja Casablanca.

Timu hiyo imeingia kambini Azam Complex Chamazi kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya timu ya Misri ya Pyramids katika mchezo wa pili utakaochezwa Dar es Salaam Machi 17, mwaka huu.

Pyramids imetoka kushinda mchezo wake wa kwanza dhidi ya Nkana kwa kuifunga mabao 3-0.

Chanzo: www.habarileo.co.tz