Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya Ligi yawaondoa waamuzi 10

Almasi Kasongooo Bodi ya Ligi yawaondoa waamuzi 10

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Ligi nchini Tanzania imesema kuwa imewaondoa waamuzi 10 wa Ligi ya Championship kutokana na kufanya makosa ya kutofuata sheria na kanuni za soka.

hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Almasi Jumapili Kasongo wakati akihojiwa na kituo cha televisheni cha TV3 kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu ligi.

"Sisi kama bodi ya ligi tunawashukuru sana TV3 katika kipindi ambacho wamekuwa na msaada mkubwa kwenye Ligi ya Championship basi ni msimu huu kwa hakika mmetusaidia sana kuonyesha hizi mechi.

"Na kutokana na nyie kuonyesha ligi hii tumekuwa tunafanya maamuzi pale tunapoona vitu vimeenda tofauti. Mpaka sasa tumewaondoa waamuzi 10 kwenye ligi na sio tu kwamba tumewaondoa kwa muda yaani hawatokuwepo tena.

"Na kwa kipindi hiki ambacho ligi inaelekea mwisho tutakuwa makini zaidi kwenye Kila mechi ili kuhakikisha timu zinashinda kw haki," amesema Almasi Kasongo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live