Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya Ligi yatoa neno Uwanja wa Ushirika

Ushrika Stadium Uwanja wa Ushirika Moshi

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imeufungulia Uwanja wa Ushirika uliopo Moshi,Kilimanjaro ili uanze kutumika kwa mechi za Ligi Kuu msimu huu.

Taarifa iliyotolewa na TPLB usiku huu imeeleza kuwa Uwanja huo unaotumika kwa mechi za nyumbani za Polisi Tanzania, umefunguliwa baada ya kukamilika kwa marekebisho yaliyohitajika kufanyika

"Uwanja huo umefanyiwa maboresho katika maeneo yote muhimu ikiwemo eneo la kuchezea (pitch), vyumba vya kuvalia na uzio unaotenganisha mashabiki na eneo la kuchezea."

"Kwa mujibu wa Kanuni ya 9:8 ya Ligi Kuu, Uwanja huo utaruhusiwa kutumika kwa michezo ya Ligi kuanzia Novemba 20, 2022 ikiwa ni siku 14 tangu ulipokaguliwa na Kamati ya Leseni za Klabu, Novemba 5, 2022," ilifafanua taarifa hiyo ya TPLB.

Katika hatua nyingine TPLB imezitaka klabu kuhakikisha klabu zinatunza viwanja vyao vya nyumbani.

"Bodi ya Ligi inaendelea kuzikumbusha klabu kuhakikisha viwanja vyao vya nyumbani vinakuwa katika hali ya ubora wakati wote ili vikidhi matakwa ya kanuni na sheria za mpira wa miguu," ilisisitiza TPLB.

Uwanja wa Ushirika ulifungiwa kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu msimu huu, jambo lililoilazimu Polisi Tanzania kutumia viwanja vya Sheikh Amri Abeid, Arusha na Black Rhino, Karatu kwa mechi zake za nyumbani

Chanzo: www.tanzaniaweb.live