Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya Ligi yatembeza rungu

Bodi Pic Data Bodi ya Ligi yatembeza rungu

Sun, 28 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Ramadhan EliasMore by this Author

RAMADHAN ELIAS KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Februari 24, 2021 ilipitia mwenendo wa matukio mbalimbali ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambapo iligundua baadhi ya mambo na kuyatolea maamuzi.

Timu ya Dodoma Jiji imepigwa faini ya Sh 500,000 kwa kosa la viongozi na wachezaji wake kushuka kwenye gari na kuingia uwanjani kinyumenyume kitendo kilichoashiria imani za kishirikina katika mchezo dhidi ya Coastal Union uliochezwa Februari 17, 2021 uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Adhabu hiyo ni kwa kuzingatia kanuni ya 45 (1) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa klabu.

KMC nayo imepewa onyo kali kwa kosa la kutotumia mlango sahihi kuingia vyumbani mara baada ya kumaliza mazoezi ya kupasha misuli joto ambapo walipita kwenye geti dogo la kuingilia uwanjani na kupita mlango wa VIP kuingia katika vyumba vyao vya katika mchezo dhidi ya Mwadui uliochezwa Februari 16, 2021 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam,  adhabu hiyo imetolewa kwa uzingativu wa kanuni ya 15(54) ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za mchezo.

Biashara United imetozwa faini ya Sh 500,000 kwa kosa la mashabiki wa timu hiyo kumrushia chupa mwamuzi msaidizi namba mbili mnamo dakika ya 31 katika mchezo dhidi ya Simba uliochezwa Februari 18, 2021 kwenye uwanja wa Karume mkoani Mara.

Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 45(1) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa Klabu.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz