Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya Ligi yasogeza mbele mechi za Yanga, Simba

Simba Yanga Bodi ya Ligi yasogeza mbele mechi za Yanga, Simba

Sat, 1 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) imetangaza kusogeza mbele baadhi ya michezo ya Ligi Kuu ya NBC ambayo inahusisha vilabu vinavyoshiriki katika michuano ya Ligi ya Mbaingwa Barani Afrika ikiwemo Yanga, Simba na Azam FC.

Mchezo wa Klabu ya Yanga dhidi ya Namungo FC, ambao ulipangwa kuchezwa tarehe 13 Oktoba, 2022 kwenye uwanja wa Majaliwa, Lindi umeahirishwa hadi pale utakapotangazwa tena.

Vivyo hivyo kwa michezo kati ya Singida Big Stars dhidi ya Simba SC na mchezo mwingine kati ya Azam FC dhidi ya Dodoma Jiji.

Bodi ya Ligi imefanya maamuzi hayo ili kuzipatia klabu hizo muda mzuri wa maandalizi, kusafiri na kushindana kikamilifu kuelekea kwenye michezo wa marudiano katika hatua ya mtoano kufuzu makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live