Bodi ya ligi chini ya Afisa Mtendaji Mkuu Almasi Kasongo, imekutana na waandishi wa habari kama njia ya kuboresha mahusiano kwa kuwa hao ndio msingi mkubwa katika kufikisha habari kwa wananchi.
Katika Warsha hiyo ajenda kuu zilikua ni mbili ambazo ni Maandalizi kuelekea msimu mpya, pili kuboresha mahusiano baina ya bodi, TFF na Waandishi wa habari.
Akizungumza katika Warsha hiyo Kasongo amesema;
"Ligi inaelekea kuanza mwishoni mwa mwezi huu, na sisi kama bodi tunataka kuhakikisha zile changamoto zote tunazipunguza ama tunazimaliza"
"Waandishi wa habari ni watu wetu wa karibu sana, wamekua wakifanya kazi nasi bega kwa bega na sisi tuwaahidi kwamba tutatoa ushirikiano,TFF wanawategemea kuhakikisha mawapa wapenda soka taarifa za mpira wetu kwa maendeleo ya soka letu" amesema Kasongo
Waandishi wa Habari vile vile walipewa mafunzo mafupi ya namna ya kuripoti shughuli mbali mbali za Michezo kiuweledi.
Ligi kuu ya Tanzania Bara, inatarajiwa kuanza Mwishoni mwa mwezi huu lakini kumekua na malalamiko kutoka kwa watu kuhusiana na suala la ratiba kutotoka mpaka wakati huu.