Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya Ligi yaipeleka Yanga uwanja wa Sokoine

Kikosi Cha Yanga Tunisia 1 1140x640 Bodi ya Ligi yaipeleka Yanga uwanja wa Sokoine

Sun, 20 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kitendo cha Bodi ya Ligi (TPLB) kuufungia Uwanja wa Highland Estaste, Mbarali, unaotumiwa na Ihefu katika michezo yake ya nyumbani Ligi Kuu, mchezo kati ya timu hiyo na Yanga utapigwa Uwanja wa Sokoine tofauti na awali kama ilivyopangwa kwenye ratiba kufanyika Highland.

Hata hivyo kufungiwa kwa uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 5,000 pekee sasa unafanya mashabiki wengi kujitokeza Sokoine ambao una uwezo wa kuingiza mashabiki 20,000.

Ihefu inayoburuza mkia kwenye ligi ikiwa na alama tano baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 nyumbani dhidi ya Polisi Tanzania ambayo imepanda hadi nafasi ya 14 ikiwa na alama tisa.

Jumapili hii Ihefu itashuka Uwanja wa Sokoine kucheza na Coastal Union ambayo wiki iliyopita iliilazimisha sare ya mabao 2-2 Mbeya City.

Hata hivyo, Meneja wa Uwanja wa Sokoine, Modestus Mwaluka alisema kwake ni furaha kuendelea kuaminiwa na kuzidi kupewa timu ambazo zinautumia uwanja.

“Kuutunza uwanja sio kazi ndogo, kila wakati uwanja unatakiwa kupata maji, mbolea na mambo mengine ambayo yataufanya uwanja kuendelea kuwa bora kila wakati na kuaminiwa na bodi ili kutumika katika michezo. “Hakuna mtu anayependa kuona uwanja wake ukifungiwa ndio maana uwanja wetu muda mwingi umekuwa kielelezo kwa viwanja vingine na kupata tuzo kila wakati kutokana na ubora wa uwanja wetu,” alisema Mwaluka.

Taarifa ya TPLB inaeleza unaufungia uwanja huo kutokana na kukosa vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu hasa eneo la kuchezea (pitch) kukosa majani ya kutosha hivyo kutokuwa salama kwa watumiaji.

Kuelekea mchezo wa kesho, kocha wa Coastal Union, Yusuf Chipo alisema makosa waliyofanya katika mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Manungu watajitahidi kuyasahihisha ili mchezo huo wapate matokeo mazuri.

“Kabla ya kupata sare na Mbeya City tulishinda mbele ya Tanzania Prisons, hivyo Uwanja wa Sokoine umekuwa na bahati kwetu ya kuondoka na alama, lakini kutokana na hali ya ushindani wa ligi ulivyo tumejiandaa kukabiliana na changamoto zitakazojitokeza,” alisema Chipo.

Chanzo: Mwanaspoti