Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya Ligi yaigomea Mamelodi Sundowns

Yangaaaa X Mamelodi Yanga vs Mamelodi

Tue, 2 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Ligi ya DStv Premiership mchini Afrika Kusini imekataa kuahirisha Mchezo wa ligi kuu baina ya Richardsbay dhidi ya Mamelodi Sundowns.

Mchezo huo wa kiporo utachezwa leo Aprili 2024 katika uwanja wa Loftus Versveld.

Katika timu (8) zilizo hatua ya Robo fainali CAF-CL 23/23, Mamelodi Sundowns ni timu pekee itakayocheza Mchezo wa ligi kuu wiki hii.

Timu zingine michezo yao ya Ligi Kuu imeahirishwa ili kujiandaa na mechi za mkondo wa pili wa robo fainali CAF Champions League.

Bodi hiyo ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini imefanya hivyo kutokana na kuwa Mamelodi wana viporo (3) kwenye Ligi Kuu.

Msimamo wa Ligi Kuu ya DStv

1. Mechi 18 alama 46 — Mamelodi

2. Mechi 20 alama 35 — Stellenbosch

3. Mechi 20 alama 33 — Sekhukhune Utd

4. Mechi 21 alama 33 — Orlando Pirates

Ikumbukwe kuwa, Mamelodi ilicheza na Yanga, Jumamosi Machi 30, 2024 katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali hizo na kutoa sare ya bila kufungana katika Dimba la Mkapa.

Yanga wataondoka leo kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Mamelodi, mechi ambayo itapigwa Ijumaa Aprili 5, 2024 katika Dimba la Loftus Versfeld, Pretoria nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live