Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya Ligi yaahirisha mechi za Simba, Yanga, Azam

Simba SC BB.jpeg Bodi ya Ligi yaahirisha mechi za Simba, Yanga, Azam

Fri, 22 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Ligi imetangaza kuhairisha mechi saba za Ligi Kuu zilizopangwa kupigwa kuanzia Desemba 26, mwaka huu ili kupisha mchezo kati ya timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) na timu ya Taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) utakaofanyika Desemba 27 mwaka huu.

 TPLB imetaja sababu nyingine yakuhairishwa kwa mechi hizo ni kupisha maandalizi ya Taifa Stars kwa ajili ya fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon 2023) nchini Ivory Coast Januari 13, 2024.

Taarifa hiyo imeeleza mchezo huo maalum (Zanzibar Heroes na Kilimanjaro Stars) uatafanyika Uwanja wa Aman- Zanzibar utatumika kufungua rasmi uwanja huo baada ya maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais wake, Dk Hussein Mwinyi.

Michezo iliyohairishwa ni; Mashujaa vs Simba (Desemba 26, 2023) Kagera Sugar vs Yanga (Desemba 26, 2023)

Tabora United vs Simba (Desemba 29,2023) Yanga vs Mashujaa (Desemba 29, 2023) Simba vs Azam (Januari 1, 2024) Geita Gold vs Simba (Januari 4,2024) Yanga vs Dodoma Jiji (Januari 2, 2024)

Michezo hiyo itapangiwa tarehe nyingine baada ya Taifa Stars kumaliza michezo yake ya Afcon 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live