Klabu ya Simba italazimika kuilipa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kiasi cha shilingi milioni moja (1,000,000) kufuatia mashabiki wa timu hiyo kumrushia chupa za maji mchezaji wa Tanzania Prisons Samson Mbangula.
Kitendo hicho kilitokea wakati Samsoni Mbangula akitoka uwanjani baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya kwa beki wa Kikongo Henock Inonga kwenye mechi ya mwisho ya Simba ya Ligi ambapo Wanalunyasi walishinda bao 7-1.
Mbali na Simba, Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi imetoa adhabu kwa klabu ya Geita Gold FC kucheza bila mashabiki kwa sasa ya watu wa timu hiyo kuingilia kati masuala ya watawala.