Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya Ligi Tanzania yaja na maazimio manne Ligi Kuu kuchezwa bila mashabiki

99466 Pic+ligi+kuu Bodi ya Ligi Tanzania yaja na maazimio manne Ligi Kuu kuchezwa bila mashabiki

Thu, 19 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Bodi ya Ligi Tanzania (TPL-Board) imeweka maazimio manne ikiwamo ligi kuchezwa bila mashabiki baada ya siku 30 za kusimamishwa kwa mashindano yote nchini.

Maazimio hayo yamefikiwa leo katika kikao cha Kamati ya uongozi na uendeshaji wa Ligi kilichofanyika jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku moja tangu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotangaza kusitisha mikusanyiko ikiwamo matukio ya kimichezo nchini kwa mwezi mmoja.

Ofisa Mtendaji wa Bodi (CEO), Almas Kasongo amesema katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Corona ulioingia nchini, wameazimia Ligi kuchezwa bila mashabiki itakapoendelea mwezi ujao.

"Tumeweka maazimio manne, Serikali ikijiridhisha hali ni shwari nchini na kuruhusu Ligi kuendelea, basi wachezaji wote watapimwa kabla ya mechi," alisema.

Alisema kingine walichoazimia ni Ligi kumalizika ndani ya mwezi Juni ili kutoa nafasi kwa timu zitakazoiwakilisha nchi kimataifa kuendelea na mchakato wa mashindano ya CAF."

Alisema kingine ni wao kuendelee kuwa maajenti wazuri kusimsamia afya kipindi hiki cha tahadhari ya Corona hivyo wameazimia Ligi ichezwe bila mashabiki mara itakapoendelea.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz