Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya Ligi: Sasa ruksa Ligi Kuu Bara kutumia viwanja vya Zanzibar

Uwanja Wa Amaan ZNZ KKK.jpeg Bodi ya Ligi: Sasa ruksa Ligi Kuu Bara kutumia viwanja vya Zanzibar

Tue, 6 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtendaji Mkuu wa Bidi ya Ligi, Almas Kasongo, ameweka wazi kwamba kuna maboresho kwenye Kanuni za ligi msimu wa 2024-25 ambapo zinaruhusu timu za Ligi kuu kutumia viwanja vya Unguja na Pemba visiwani Zanzibar ikiwa vitakidhi vigezo.

Aidha, Kasongo amesema kuwa baadhi ya kanuni za ligi msimu ujao wa 2024/25 ni kuwa uwanja ambao hautakuwa na viti elfu tatu (3,000) kwa ajili ya mashabiki havitatumika kwenye michezo ya Ligi Kuu.

“Jana nimepokea barua ya timu ya Ligi Kuu kutumia uwanja wa Zanzibar kama uwanja wao wa nyumbani. Timu yeyote ya Tanzania Bara, ikiamua kutumia uwanja wowote visiwani (Unguja/Pemba) ruksa,” amesema Kasongo.

Itakumbukwa kuwa, msimu uliopita Simba iliandika barua kwa Bodi ya Ligi kuomba uwanja wa Amaan kuwa uwanja wao wa nyumbani, lakini kulingana na kanuni za ligi zilizokuwepo, Simba haikuruhusiwa kutumia uwanja huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live