Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya Ligi: Hatupangui ratiba

Azam Simba Sz Bodi ya Ligi: Hatupangui ratiba

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara imesema haitaraji kufanya mabadiliko ya ratiba kutokana na ushiriki wa timu za Simba na Yanga kwenye michezo ya Kimataifa, kwani Kila kitu kimewekwa sawa.

Akizungumza nasi jijini leo Ofisa habari wa Bodi hiyo Karim Boimanda alisema ratiba inawapa nafasi Simba na Yanga kushiriki mashindano hayo mpaka mwisho,labda yatokee mabadiliko yatakayowalazimu wabadilishe ratiba hiyo.

"Tutarajie ratiba ikitekelezwa vizuri bila kuwa na michezo ya viporo malengo yetu ni kuona Ligi inamalizika kwa wakati na hatutarajii kuwa na viporo vingi," alisema Boimanda.

Alizitaka Klabu zote kufuata kanuni na sheria za Ligi kwani wakifanya hivyo wataiboresha zaidi Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live