Bodi ya Ligi Kuu imetengaza mechi zote za mwisho kumalizia msimu Juni 9 zitachezwa saa 9:30 alasiri badala ya saa 10:00 jioni.
Katika taarifa waliyotoa Bodi ya Ligi wamesema mechi zote zitapigwa muda huo kwasababu kutakuwa na sherehe za kukabidhi kikombe cha ubingwa kwa Yanga itakayocheza Uwanja wa Sokoine dhidi ya Tanzania Prisons.
Katika hatua nyingine Bodi ya Ligi imeonya klabu kuepuka vitendo vinavyoashiria upangaji wa matokeo na kuhamasisha mchezo wa kiungwana.
"Kanuni ya 33 ya Ligi Kuu inazungumzia athari hasi na adhabu kali zinazoweza kutolewa kwa chama cha mpira cha mkoa, klabu, viongozi, wachezaji au mdau yeyote atakayebainika kuwa ameshiriki kwa namna yoyote kupanga matokeo ikiwemo kula njama, kushawishi, na kutekeleza jambo lenye kuchafua taswira ya mchezo wa soka," imeeleza taarifa hiyo.