Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodaboda wateka gwaride la Yanga

Boda Boda Gwaride Bodaboda wateka gwaride la Yanga

Sat, 10 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Madereva mbalimbali wa Bodaboda wamejitokeza kwa wingi katika gwaride la Yanga la kusherehekea ubingwa wa 29 wa Ligi Kuu Bara.

Katika mapokezi hayo bodaboda wameonekana kwa wingi huku wakiimba nyimbo mbalimbali za kuisapoti timu hiyo baada ya kutwaa taji hilo.

Katika maeneo ya Vingunguti ambapo gwaride hilo linaendelea kwenda hadi Jangwani, mashabiki hao wamejitokeza huku wakiwa wamevalia jezi za Yanga na kuimba nyimbo mbalimbali huku wakipiga mavuvuzela.

Yanga imetua leo jijini Dar es Salaam ikitokea Mbeya ilikohitimisha msimu jana na kukabidhiwa taji hilo la 29, baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Maafande wa Tanzania Prisons.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: