Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bocco yuko fiti, kuwakabili TP Mazembe kwa Mkapa

Bocco2 660x400.jpeg Nahodha wa Simba, John Bocco

Fri, 10 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kinara wa ufungaji Ligi kuu Bara msimu wa 2020/2021, John Rafael Bocco, yuko fiti kuwavaa TP Mazembe kwa Mkapa Septemba 19, ambayo ni siku ya kilele cha Simba Day.

Hiyo ni baada ya kupona majeraha yake ya enka yaliyomfanya aondolewe kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichocheza dhidi ya DR Congo Septemba 2 na Madagascar katika kuwania kufuzu Kombe la Dunia kule Qatar 2022.

Septemba 19, mwaka huu, Simba itavaana na TP Mazembe katika mechi ya kirafiki itakayochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar kwenye Tamasha la Simba Day.

Mratibu wa Simba, Abbas Ally, amesema; “Bocco yupo kambini, alikuwa nje ya uwanja kwa ajili ya matibabu ya haraka ili kuhakikisha anarejea uwanjani mapema.

“Bocco amepona majeraha yake na leo (jana) asubuhi alianza mazoezi mepesi ya binafsi,” amesisitiza Ally

Chanzo: www.tanzaniaweb.live