Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bocco gari limewaka, Pablo atoa neno

Bocco B Bocco alifunga magoli mawili katika ushindi dhidi ya Ruvu Shooting

Sat, 19 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco amesifu kiwango kilichoonyeshwa na mshambuliaji wake John Bocco katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) hatua ya 16, dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kauli ya Pablo inakuja baada ya nahodha huyo wa Simba kufunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 7-0, kuondoa gundu la kukaa kwa muda mrefu bila ya kufunga tangu alipofanya hivyo kwa mara ya mwisho katika ushindi wa mabao 4-0, dhidi ya Namungo FC Julai 18, 2021.

“Wote tunayofuraha kuona amefunga na kuisaidia timu kuvuka hatua inayofuata, ni jambo jema kwake maana itamuongezea hali nzuri ya kujiamini katika michezo yetu ijayo,” alisema Pablo na kuongeza;

“Changamoto ya kukaa muda mrefu bila ya kufunga humtokea mshambuliaji yeyote hivyo kwetu kama benchi la ufundi hatuna shaka na uwezo wake ndio maana tuliendelea kumwamini na kumpatia nafasi ya kucheza na mwishowe ameweza kufunga.”

Mchezo huo ni wa pili kwa nyota huyo kuonyesha kiwango bora baada ya kutoa pasi ya bao la tatu la Peter Banda katika ushindi wa 3-1, dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast katika Kombe la Shirikisho Afrika Februari 13 kwenye Uwanja wa Mkapa.

Simba ikiwa imecheza mechi 15 za Ligi Kuu Bara, imefunga jumla ya mabao 16 huku mshambuliaji wake hatari Meddie Kagere akiwa ndiye kinara akifunga matano, huku Bocco akiwa bado hajafunga bao kwenye michuano hiyo licha ya msimu uliopita kuibuka na tuzo ya mfungaji bora akiwa na mabao 16.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live